Paris Masters: Murray amtupa nje Verdasco

Murray amekuwa katika kiwango kizuri hivi karibuni
Image caption Murray amekuwa katika kiwango kizuri hivi karibuni

Muingereza Andy Murray amemtupa nje Mhispania Fernando Verdasco katika michuano ya Paris Masters raundi ya pili.

Murray mwenye miaka 29, ambaye anaweza kumpiku Novak Djokovic akiwa na msimu mzuri wiki hii, ameshinda kwa seti 6-3 6-7 7-5 katika mchezo uliodumu kwa masaa mawili na dakika 29.

Mapema Djokovic alimbwaga Gille Muller kwa seti 6-3 6-4, Mserbia huyo atasalia kuwa namba 1 kwa ubora duniani kama ataweza kufika fainali.

Andy Murray anatarajia kuwa mchezaji wa kwanza namba moja mwenye umri mkubwa kwa mara ya kwanza tangu Muastralia John Newcombe alipofanya hivyo mwaka 1974 akiwa na umri wa miaka 30.