Manny Pacquiao arudi ulingoni na ushindi

Manny Pacquiao arudi kwa kishindo kikubwa Las Vegas
Image caption Manny Pacquiao arudi kwa kishindo kikubwa Las Vegas

Bingwa wa zamani katika uzani wa Welterweight duniani Manny Pacquiao alirudi katika ulingo wa ndondi kwa kishindo kikubwa baada ya kumshinda kwa wingi wa pointi bingwa Jessie Vergas na kushinda taji la Welterweight mjini Las Vegas.

Pacquiao menye umri wa mika 37 alitangaza kustaafu baada ya kumshinda Timothy Bradley mnamo mwezi Aprili.

Majaji waliandikisha pointi 114-113,118-109 na 118-109 kwa upande wa raia huyo wa Ufilipino.

Aliyekuwa mpinzani wake mkubwa katika uzani huo Floyd Mayweather alihudhuria pigano hilo.

Image caption Manny Pacquiao akimpiga makonde makali mpinzani wake

''Si mbaya'',alisema Mayweather na kumpongeza Pacquiao kwa kushinda pigano hilo.

Mayweather alimshinda Pacquiao ili kushinda taji hilo mnamo mwezi Mei 2015 katika kile kilichotajwa kuwa pigano la ''karne'' hii.

''Nilimualika kuhudhuria pigano hili usiku huu'' ,alisema Pacquiao. Alipoulizwa iwapo wawili hao wanaweza kukutana tena ,alijibu 'tutaona'.