Arsenal yatoka sare na Tottenham

Arsenal yatoka sare na Tottenham uwanjani Emirates
Image caption Arsenal yatoka sare na Tottenham uwanjani Emirates

Harry Kane alionyesha umahiri wake baada ya kuuguza jereha kwa majuma saba kwa kufunga bao la kusawazisha dhidi ya wenyeji Arsenal katika uwanja wa Emirates,na kuifanya Tottenham kusalia kuwa timu ambayo haijafungwa katika ligi ya Uingereza msimu huu.

Mshambuliaji huyo wa Uingereza alikuwa akiuguza jereha tangu tarehe 18 mwezi Septemba lakini alifunga bao la kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti mapema katika kipindi cha pili baada ya Kevin Wimmer kujifunga dakika tatu kabla ya kipindi cha mapumziko.

Arsenal ilijua kwamba ushindi utaiweka timu hiyo kileleni mwa ligi na karibia Theo Walcot aiweke kifua mbele timu yake pale mkwaju wake ulipogonga chuma cha goli,kabla ya Wimmer kuigusa na kichwa krosi iliopigwa na Ozil na kujifunga .