Koeman: Lukaku ataondoka ili atimize ndoto yake

Romelu Lukaku na mkufunzi wake Ronald Koeman
Image caption Romelu Lukaku na mkufunzi wake Ronald Koeman

Romelu Lukaku atahitajika kuondoka Everton ili kutimiza ndoto yake kulingana na meneja Ronald Koeman.

Mshambuliajj huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na Tofees kwa mkopo mwaka 2013 kabla ya kujiunga rasmi na klabu hiyo kwa kitita kilichovunja rekodi cha pauni milioni 28 mwezi Julai 2014.

Baada ya kuwasilisha ombi la kuhama msimu uliopita ,Lukaku amefunga mabao saba kati ya 15 yaliofungwa na Everton katika ligi msimu huu.

''Uwezo wake ni mkubwa na juu zaidi ya Everton'' ,alisema Koeman.

Image caption Romelu lukaku

''Iwapo Romelu angeendelea kucheza Everton hadi mwisho wa wakati wake najua angewacha kitu nyuma'', aliongezea raia huyo wa Uholanzi mwenye umri wa mika 53.

''Nilimpatia motisha na akatambua kuwa ni muhimu sana kwa ukuaji wake kuchezea Everton mwaka mwengine'' .

''Baada ya msimu huu hakuna anayejua litakalotokea''.

Everton imesema kuwa iko tayari kumpatia Lukaku kandarasi ya muda mrefu na kumfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi katika klabu hiyo.