Marekani kucheza dhidi ya Mexico

Gazeti la Mexico Haki miliki ya picha Reuters
Image caption 'Mungu Wangu!', ushindi wa Trump haujapokelewa vyema Marekani

Ushindi wa mgombea wa Republican Donald Trump uchaguzi wa urais Marekani umeongeza uzito kwenye mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia kati ya Marekani na Mexico itakayochezwa Ijumaa, nahodha wa Marekani Michael Bradley amesema.

Trump, wakati wa kampeni alisema Wamexico ni "wahalifu" na anataka kujenga ukutaza mpakani kuwazuia raia wa Mexico kuingia Marekani.

Mechi hiyo itachezewa jimbo la Ohio, jimbo la kushindaniwa ambapo Trump aliibuka na ushindi.

Bradley anasema mashabiki watakaohudhuria mechi lazima waheshimiwe, wawe "Wamarekani, Wamexico, watu wasioegemea upande wowote, wanawake, wanaume au watoto".

Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto awali amemtuhumu Twump kwa kuharibu uhusiano wa Marekani na Mexico, baada ya Twump ksuema wahamiaji wa Mexico walio Marekani bila vibali ni "wahalifu" na "wabakaji".

Aidha, Trump alisema Mexico italipia kujengwa kwa ukuta wa kuzuia wahamiaji mpakani, madai ambayo serikali ya Mexico imepuuzilia mbali.

Kipa wa Marekani Tim Howard amesema anatumai mechi hiyo mjini Colombus haitagubikwa na siasa.

Ijumaa itakuwa mwanzo wa hatua za mwisho za kufuzu kwa Kombe la Dunia nchi za kanda ya Concacaf, ambapo timu sita - Marekani, Mexico, Costa Rica, Trinidad & Tobago, Honduras na Panama - zinashindania nafasi tatu za kufuzu moja kwa moja kwa Kombe la Dunia Urusi 2018.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii