Watakaopigania tuzo ya mwanasoka bora zaidi Afrika 2016

Piga kura sasa

Wachezaji watano watakaoshindania Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka 2016 wametangazwa.

Wachezaji hao ni Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Riyad Mahrez, Sadio Mane and Yaya Toure.

Wachezaji hao watano walitangazwa wakati wa kipindi maalum cha moja kwa moja runingani Jumamosi.

Piga kura hapa : bbc.com/africanfootball

Mshindi atachaguliwa na mashabiki wa soka ya Afrika kutoka kila kona ya dunia. Mashabiki wana hadi saa 18:00 GMT tarehe 28 Novemba kumpigia kura mchezaji wanayempenda.

Mnamo Jumatatu, 12 Desemba, mshindi wa tuzo hiyo atatangazwa moja kwa moja kwenye runinga ya BBC Focus on Africa pamoja na redio, kuanzia saa 17:35.

Tovuti za BBC Swahili, BBC Sport na BBC Africa pia zitachapisha habari za mshindi.

Aubameyang ameorodheshwa kwa mwaka wan ne mtawalia, mshindi wa mwaka 2011 pia ameorodheshwa kwa mwaka wa nne, Mahrez ndiye mchezaji pekee ambaye hajawahi kuorodheshwa kushindania, Mane alishindania mara ya kwanza mwaka jana naye mshindi mara mbili. Toure ameorodheshwa kwa mwaka wa nane mtawalia.

Haki miliki ya picha CARMEN JASPERSEN
Image caption Aubameyang ni mmoja wa wafungaji mabao hatari zaidi Bundesliga

Mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Aubameyang amekuwa na kipindi cha kufana sana mwaka 2016, amefunga mabao 26 (kufikia wakati wa kuandika makala hii) katika klabu yake ya Borussia Dortmund nchini Ujerumani

Alikuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika kutawazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Bundesliga, raia wa kwanza wa Gabon kushinda Tuzo ya Shirikisho la Soka Afrika ya mchezaji bora wa mwaka Afrika, na ameorodheshwa miongoni mwa wachezaji wanaoshindania tuzo ya mchezaji bora duniani mwaka 2016, tuzo ya Ballon d'Or.

Haki miliki ya picha Michael Regan
Image caption Mashabiki wa West Ham wanatumai Ayew atawafaa msimu huu

Mwezi Agosti West Ham walivunja rekodi yao ya kununua wachezaji, walipolipa Swansea £20.5m kumchukua nyota wa Ghana Ayew, ishara tosha ya kiwango kizuri cha kiungo huyo wa kati mwaka mmoja uliopita.

Ayew amekuwa akicheza vyema sana, na magoli 12 aliyoyafunga msimu wa 2015/16 mechi 35 alizochezea Swansea, ulimfanya kuitwa mchezaji bora mgeni wa klabu hiyo wakati wa tuzo za mwisho wa msimu mwezi Mei.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mahrez alikuwa mchezaji bora Ligi ya Premia msimu uliopita

Mchezaji mwingine wa Ligi Kuu ya England anayechezea Leicester City, Mahrez kutoka Algeria alifana sana na kutekeleza mchango mkubwa kwa klabu yake - ambayo uwezekano wake wa kushinda mwanzo wa msimu ulikuwa 5,000-1- na kuiwezesha kushinda ligi mara ya kwanza.

Mahrez alifunga mabao 17 ligini msimu wa 2015/16 na alichaguliwa na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa Uingereza kuwa Mchezaji Bora wa mwaka - Mwafrika wa kwanza kushinda tuzo hiyo.

Kadhalika, aling'aa na kusaidia Algeria kufuzu kwa Kombe la Taifa Bingwa Afrika 2017.

Haki miliki ya picha PAUL ELLIS
Image caption Mane huwa 'hashikiki' anapokuwa katika fomu yake

Mshambuliaji wa kimataifa kutoka Senegal Mane aliibuka mchezaji ghali zaidi katika historia ya soka Afrika aliojiunga na Liverpool kwa £34m majira ya joto mwaka huu.

Uchezaji wake ulidhihirika mara moja uwanjani Anfield, ambapo aliwafungia Liverpool mabao sita na kusaidia ufungaji wa mengine manne katika mechi 11. Ni kama aliendeleza kutoka alipoachia Southampton, ambapo alikuwa amefunga mabao manane ligini akichezea Saints mwaka 2016, ikiwa ni pamoja na mabao matatu aliyoyafunga dhidi ya mabingwa wa wakati huo Manchester City,

Haki miliki ya picha OLI SCARFF
Image caption Yaya Toure ameng'aa tangu aanze soka ya kulipwa miaka 15 iliyopita

Toure alijishindia kombe jingine mwaka 2016, kombe lake la 17 katika maisha yake ya uchezaji, aliposhinda Kombe la Ligi Uingereza akiwa na Manchester City, ambapo alifunga penalti ya ushindi wakati wa matuta dhidi ya Liverpool kwenye fainali.

Huu ulikuwa mwaka ambao kigogo huyu wa safu ya kati kutoka Ivory Coast, ambaye sasa ana miaka 33, alistaafu soka ya kimataifa baada ya ufanisi mkubwa lakini bado akajidhihirisha kwamba hajaishiwa na nguvu ya kucheza na kujumuishwa kwenye orodha hii kwa mwaka mwingine kunatilia mkazo hili.

Piga kura hapa : bbc.com/africanfootball

Mada zinazohusiana