Kanuni na Masharti ya Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka 2016

Kanuni na Masharti ya Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka 2016

Orodha ya wachezaji watakaopigania Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka 2016 itatangazwa kwenye kipindi maalum cha moja kwa moja cha Mchezaji wa Afrika wa Mwaka katika BBC World Service, BBC World News, mitandao ya BBC na katika mitandao ya kijamii. Kipindi hiki kitapeperushwa saa 1805GMT hadi 1900 GMT mnamo Jumamosi Novemba 12. Ukurasa wa kupigia kura utafunguliwa takriban saa 1850GMT.

Maelezo na utaratibu wa kupiga kura ni kama ifuatavyo.

Shughuli ya kuchagua wachezaji wa kushindania

Orodha ya wachezaji watano wa kushindania tuzo hii ilitayarishwa na wataalamu bingwa wa soka Afrika, ambapo mtaalamu mmoja kutoka kila nchi aliombwa kutaja wachezaji watatu anaohisi wanafaa kushindania, bila kufuata utaratibu wowote katika kuwataja wachezaji hao watatu.

Waliombwa kuteua wachezaji wao kwa kufuata mambo yafuatayo: ustadi wa kibinafsi; uwezo wa kiufundi; kufanya kazi na timu; mchango katika matokeo na kucheza kwa njia ya haki, zilizoonyeshwa wakati wa msimu wa 2015/16.

Majina ya wachezaji watakaoshindania tuzo yatatangazwa wakati wa kipindi cha moja kwa moja runingani na redioni mnamo Jumamosi 12 Novemba kuanzia saa 1805-1900 GMT katika BBC World Service na BBC World TV. Majina yatatangazwa pia katika www.bbc.com/africanfootball.

Ikitokea kwamba kuwe na wachezaji waliotoshana kwa kura wakati wa uteuzi, kundi la waandalizi wa Tuzo ya Mwanakandanda Bora wa Mwaka wa Afrika ina haki ya kuongeza orodha ya wachezaji wa kushindania tuzo hadi wachezaji sita.

Nani anastahili kushindania

Watu wamehitimu kushindania Tuzo ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka iwapo wanahitimu kuchezea timu ya taifa lolote la Afrika.

Umma kupiga kura

Majina ya wachezaji watakaoshindania tuzo yatakapochapishwa, mshindi wa tuzo ataamuliwa kupitia kura za umma mtandaoni.

Shughuli ya upigaji kura itafunguliwa takriban saa 1850 GMT mnamo Jumamosi 12 Novemba 2016 na kufungwa saa 1800 GMT mnamo Jumatatu 28 Novemba 2016.

Matokeo ya mwisho yatatangazwa saa 17:35 GMT mnamo Jumatatu Desemba 12, moja kwa moja katika runinga ya Focus on Africa na redio. Mshindi pia atatangazwa kwenye ukurasa wa Mchezaji Bora wa Afrika wa BBC pamoja na kanuni na masharti yanayotumika.

Ikitokea kwamba wachezaji watoshane kwa kura, wachezaji hao watatunukiwa tuzo kwa moja.

Jinsi ya kupiga kura - mtandaoni

Kwa kutembelea ukurasa wa Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka katika www.bbc.com/africanfootball na kufuata maagizo mtandaoni. Kompyuta moja inaweza tu kutumiwa kupiga kura mara moja.

Kura ya umma - Kanuni na masharti

1. Kura hii inaendeshwa na BBC na tuzo hii imetimiza viwango na matakwa ya mwongozo wa maadili wa BBC kuhusu kufanywa kwa mashindano & kura ambao unaweza kupatikana www.bbc.co.uk/editorialguidelines/guidelines/appendix2

2. Mshindi atapokezwa kikombe kilichoandikwa jina na atunukiwe taji la Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka wa BBC 2016.

3. Orodha ya wachezaji watakaoshindania Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka itaandaliwa na wataalamu wa soka kutoka Afrika.

4. Utaratibu uliofuatwa kupata majina haya ni kama ifuatavyo: ustadi wa kibinafsi; uwezo wa kiufundi; kufanya kazi na timu; mchango katika matokeo na kucheza kwa njia ya haki, zilizoonyeshwa mwaka 2016.

5. Majina ya wanaoshindania tuzo yatawekwa wazi kwa umma wapigiwe kura kupitia tovuti ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka katika www.bbcworldservice.com/africanfootballer na www.bbc.com/africanfootball. Kompyuta moja itaruhusiwa kupiga kura moja pekee mtandaoni..

6. BBC itatumia maelezo ya mtu binafsi kwa minajili ya kufanikisha upigaji kura pekee na haitayachapisha au kuyawasilisha kwa mtu mwingine yeyote yule bila idhini yako. Iwapo ungependa kufahamu zaidi kuhsuu sera ya faragha ya BBC, tafadhali tazama Sera ya Faragha ya BBC katika www.bbc.co.uk/usingthebbc/privacy.

7. Muda wa mwisho kupiga kura ni saa 1800 GMT mnamo Jumatatu 28 Novemba 2016.

8. Uamuzi kuhusu kura zitakazopigwa ni wa mwisho na hakutakuwa na mawasiliano ya ziada..

9. Tuzo lazima ipokelewe kama ilivyoelezwa na haiwezi kuahirishwa. Hakutakuwa na malipo yoyote ya kifedha mbadala. Hakutakuwa na malipo kwa sababu ya kupiga kura.

10. BBC, watu waliopewa kandarasi na BBC, kampuni tanzu na/au mawakala hawawezi kukubali lawama kwa matatizo yoyote ya kiufundi au matatizo mengine yoyote kuhusiana na kufikia huduma ya mtandao, mfumo wa mtandao, sava, mtoaji huduma ya mtandao au mambo mengine ambayo huenda yakasababisha kura kupotea au kutonakiliwa au kusajiliwa vyema.

12. BBC inabaki na haki ya kubatilisha kura zilizowasilishwa au kusitisha upigaji kura kukitokea sababu za kutosha za kushuku kwamba ulaghai umetokea katika upigaji kura au ikishuku kwamba kumekuwa na jaribio la wizi wa kura. BBC ina haki ya kutoa njia mbadala ya kufanya uteuzi bila kuomba ushauri kutoka kwingineko. BBC haitachapisha habari na maelezo au kuwasilisha maelezo hayo kwa mtu yeyote bila idhini, ila tu katika hali ambapo yanahitajika katika kutekeleza masharti haya. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tazama: Sera ya Faragha ya BBC http://www.bbc.co.uk/usingthebbc/privacy/

13. Wale wanaoshiriki katika kura hii, wote wanachukuliwa kwamba wamekubali kanuni hii na wanafungamanishwa nazo. Tafadhali, fahamu kwamba mfanyakazi wa BBC au mtu mwingine yeyote ambayo naahusika kwa njia moja ama nyingine katika maandalizi ya utoaji wa Tuzo hii haruhusiwi kupiga kura.

14. Upigaji kura wote utasimamiwa na BBC Africa.

16. BBC inabaki na haki ya kumuondoa mchezaji yeyote anayeshindani au kutokabidhi tuzo iwapo itabaini, kwa uamuzi wake mwenyewe, kwamba mchezaji huyo kuendelea kushiriki au tuzo hiyo kutolewa, kunatishia kuishushia hadi BBC.

17. Kanuni hizi zimo chini ya sheria za England na Wales.

Mada zinazohusiana