AFOTY: Wasifu wa Yaya Toure

Huwezi kusikiliza tena
Yaya Toure, kigogo wa Manchester City

Yaya amewahi kushinda Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka mara mbili na ni mshindi mara nne wa taji la mchezaji bora wa mwaka wa taji linalotolewa na shirikisho la soka barani Afrika (CAF), kwa hivyo haishangazi kumuona tena katika orodha ya wanaogombea taji hilo.

Anaweza kuwa alicheza mara 23 pekee mwaka 2016 na mara moja msimu huu lakini uteuzi wake unaonyesha umuhimu wake katika soka ya Afrika.

Na hata kama anaendelea kucheza, mchango wake unatambulika.

Mnamo mwezi Februari aliishindia klabu yake ya Manchester City kombe la Ligi alipofunga penalti ya pekee kuishinda Liverpool katika fainali.

Pia ameisaidia klabu yake kufika robo fainali Kombe la Klabu Bingwa Ulaya na kumaliza katika nafasi ya nne katika ligi ya Uingereza ili kuhakikisha kuwa timu hiyo inawakilishwa tena Kombe la Klabu Bingwa Ulaya .

Ufanisi huo ulimaanisha kwamba Toure aliamua kusalia na kupigania nafasi yake katika kikosi cha City licha ya kuwasili kwa Pep Guardiola ambaye alichangia kuondoka kwake katika timu ya Barcelona wakati alipokuwa mkufunzi wa timu hiyo.

Lakini wakati matamshi ya ajenti wake Dimitri Seluk kwamba mchezaji huyo ananyanyaswa wakati alipoachwa nje katika kikosi cha michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya msimu huu, mchezaji huyo aliachwa nje kabisa ya kikosi cha Manchester City na hajakuwa akichezeshwa.

Mkufunzi huyo alisema kuwa Toure hatoshiriki mechi za klabu hiyo hadi pale ajenti wake atakapoomba msamaha, ijapokuwa hilo halijatekelezwa, Toure mwenyewe ameomba msamaha.

Ijapokuwa Toure hapendezwi na hatua ya kuwekwa nje ya kikosi cha City, uamuzi wake wa kurudi katika soka ya kimataifa mwaka 2016 ni wake mwenyewe.

Alichukua takriban miezi 18 kufanya uamuzi huo kufuatia ushindi wa taifa lake katika michuano ya mataifa ya bara Afrika huko Equatorial Guinea.

Kocha wa zamani wa timu ya taifa lake Francois Zahoui alikuwa mongoni mwa wale walio jaribu kumshawishi kuendelea na harakati za kuisaidia timu yake ya taifa kufuzu kwa kombe la mataifa ya bara Afrika 2017 nchini Gabon pamoja na kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Urusi.

Sio vigumu kujua kwa nini.

Huku akiwa amechezea timu yake ya taifa mara nyingi zaidi ,Toure amekuwa kiungo muhimu katika timu ya Ivory Coast na aliimarisha ufanisi wake katika timu ya taifa kwa kuisaidia kushinda taji la Afrika la mwaka 2015.

Pia ameshiriki katika kila mechi ambayo Ivory Coast imecheza ikiwemo kushiriki mara tatu kwa timu hiyo katika michuano ya Kombe la Dunia.

Ni mwaka 2016 alipogundua kwamba ni wakati wa kustaafu katika soka ya kimataifa ijapokuwa hajatoa uamuzi wake wa mwisho.

„Ujumbe huo ulikuwa mgumu katika maisha yake," ,alisema katika taarifa yake ya kustaafu Septemba iliopita.

Lakini aliweka wazi kwamba hafikirii kwamba mchezo wake unaendelea kudorora.

''Suala kwamba mimi nina umri wa miaka 33, ugumu wa mazoezi na wingi wa mechi sio sababu kwamba ninachukua uamuzi huu," alisema.

Piga kura hapa : bbc.com/africanfootball

Mada zinazohusiana