Matumaini ya Wales kombe la dunia yazimwa

Muda mfupi baada ya Bale kupiga mwamba wa goli,Mitrovic alifunga na kuwanyamazisha mashabiki wa Wales waliojaa katika uwanja wa Cardiff. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Muda mfupi baada ya Bale kupiga mwamba wa goli,Mitrovic alifunga na kuwanyamazisha mashabiki wa Wales waliojaa katika uwanja wa Cardiff.

Matumaini ya Wales ya kufuzu katika kombe la dunia mwaka 2018 yalitiwa dosari baada ya bao la kusawazisha la Aleksandar Mitrovic wa Serbia kuwanyima ushindi huko Cardiff.

Licha ya wageni hao kucheza vizuri ,Gareth Bale aliwapatia Wales bao la kwanza baada ya mshambuliaji Hal Robson Kanu kumfanya Matija Nastasic kufanya makosa.

Mechi hiyo ilikuwa ya kuvutia huku timu zote mbili zikifanya mashambulizi katika ngome ya upinzani.

Lakini muda mfupi baada ya Bale kupiga mwamba wa goli,Mitrovic alifunga na kuwanyamazisha mashabiki wa Wales waliojaa katika uwanja wa Cardiff.

Huku taifa la Ireland likiwa limepata ushindi dhidi ya Austria na hivyobasi kupanda hadi kilele cha kundi D,Serbia na Wales wako katika nafasi ya pili na ya tatu ,wakiwa na alama mbili na nne nyuma ya kikosi cha Martin O'Neill.