Rooney amuahidi jezi kijana anayeugua saratani

Kijana anayeugua saratani amekuwa akifanyiwa kampeni katika mitandao ya kijamii Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kijana anayeugua saratani amekuwa akifanyiwa kampeni katika mitandao ya kijamii

Nyota wa timu ya soka ya Uingereza Wayne Rooney ameahidi kumpatia jezi yake mtoto anayeugua kufuatia ushindi dhidi Scotland England.

Kijana huyo amekuwa akifanyiwa kampeni katika mitandao ya kijamii.

Kasabian Newton-Smith mwenye umri wa miaka 8 kutoka Sheffield alipatikana na saratani alipokuwa mchanga na sasa ana uvimbe mara mbili katika kichwa chake.

Klabu za soka,wachezaji na watu binafsi wametakiwa kuchapisha ujumbe wa Twitter #1LastSmile4Kasabian.

Katika ujumbe wa kanda ya video,nahodha huyo wa Uingereza alisema kuwa wachezaji wenzake wanajivunia na ujasiri ulioonyeshwa na Kasabian.