Usain Bolt kujiunga na Borussia Dortmund

Bingwa wa mbio za mita 100 duniani Usain Bolt
Image caption Bingwa wa mbio za mita 100 duniani Usain Bolt

Klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund imesema kuwa mwanariadha wa mbio fupi kutoka Jamaica Usain Bolt atashiriki mazoezi na klabu hiyo kwa siku chache.

Bolt amekuwa akisema kwamba angependa kucheza soka baada ya kustaafu katika riadha.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mashabiki wa klabu ya Borussia Dortmund

Lakini wakimkaribisha, maafisa wa klabu hiyo wamesema kuwa hakuna hakiksho kwamba mwanariadha huyo ataichezea klabu hiyo katika siku za usoni.