Mshambuliaji wa Hull City kutocheza kwa mwaka mmoja

Will Keane Haki miliki ya picha Reux Features
Image caption Will Keane

Mshambuliaji wa Hull City, Will Keane hatocheza soka kwa miezi 12 kutokana na jeraha la goti.

Keane , 23, alipata jeraha hilo katika mechi dhidi ya Southampton ambayo walipata ushindi wa mabao 2-1 na atafanyiwa upasuaji siku ya Jumanne.

Mshambuliaji huyo aliejiunga na Hull City kutoka Manchester United tarehe 30 mwezi Agosti ameshiriki mechi 6 kwa upande wa Mike Phelan.

''Kumpoteza mchezaji wenye kiwango kama cha Will kwa muda mrefu ni pigo kubwa '', Phelan ameiambia tovuti ya klabu hiyo.

Hull, kwa hivi sasa iko katika nafasi ya 18 katika ligi ya premia , pointi moja nyuma ya WestHam