Steven Gerrard atarejea Liverpool kucheza?

Steven Gerrard Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Steven Gerrard

Beki wa zamani wa klabu hiyo Mark Lawrenson amesema Liverpool inastahili kumpatia mkataba Steven Gerrard kama mchezaji na meneja akisema jambo hilo litakuwa bora zaidi.

Gerrard, 36, anaondoka klabu ya LA Galaxy ya jiji la New York ambayo hucheza ligi ya MLS.

Lawrenson, anapendekeza Gerrard 'kujiunga na timu ya Liverpool' na kutumiwa kama mkufunzi katika timu hiyo.

"Hawatahitajika kumlipa maelfu ya pesa-wanaweza kumshirikisha timu hiyo,''amesema Lawrenson.

"Litakuwa jambo muhimu kumuweka mchezaji huyo karibu na klabu hiyo, kwa sababu hatachukuliwa na kama tishio na Klopp akiwa kwenye benchi la kiufundi, kwa hivyo hili si jambo la kuwa na wasiwasi nalo. Ninahakika Klopp atafurahia pia, ni jambo ambalo litaleta faida.'' Lawrenson amesema.

Gerrard alihudumu kama mkufunzi kwa timu ya Liverpool ya vijana wenye umri chini ya miaka 16 kwa muda mwaka 2015 na aliifurahia kazi hiyo, aliongeza Lawrenson.