Nigeria yaiadhibu Mali 6-0 kombe la Afrika wanawake

Oshoala alikuwa katika kiwango cha hali ya juu na kuisambaraisha ngome ya Mali
Image caption Oshoala alikuwa katika kiwango cha hali ya juu na kuisambaraisha ngome ya Mali

Asisat Oshoala alifunga magoli manne kwa timu yake ya Nigeria na kuanza vyema kampeni za kutetea taji lake la kombe la mataifa ya Afrika kwa upande wa kina dada.

Nigeria walifanikiwa kuwatandika wapinzani wao Mali goli 6-0 kikiwa ni kipigo cha aina yake.

Mchezaji bora kwa mashindano ya mwaka 2014 Oshoala alikuwa katika kiwango cha hali ya juu na kuisambaraisha ngome ya Mali.

Francisca Ordega anayechezea nchini Marekani na Uchechi Sunday wote walizifungia timu zao.

Katika mchezo unaofuata Nigeria watamenyana na mahasimu wao wakubwa wa ukanda wa Magharibi Ghana siku ya Jumatano.