WADA: Urusi haijabadilika kimichezo

Ripoti ya pili na ya Mwisho itatolewa mwezi ujao juu ya udaganyifu wa Urusi katika michezo
Image caption Ripoti ya pili na ya Mwisho itatolewa mwezi ujao juu ya udaganyifu wa Urusi katika michezo

Rais wa shirikisho la kimatifa la kupambana na dawa za kusisimua misuli WADA, amesema kuwa bado michezo ya nchini Urusi haijashawishi Dunia kuwa imebadilika.

Akiongea katika mkutano wa WADA mjini Glasgow Craig Reedie amesema wakati kunafanyika maendeleo baadhi ya miji ya Urusi bado imefungiwa na wachunguzi kutoka shirika hilo.

Mkuu mpya wa kupambana na dawa za kusisimua misuli nchini Urusi Vitaly Smirnov amekanusha kuwa walitetea mfumo wa kutumia dawa za kusisimua misuli na kusema kuwa ni tatizo la Dunia nzima.

Wanariadha na watunisha misuli wa Urusi walipigwa marufuku kushiriki katika michezo ya Olimpiki ya mwaka huu mjini Rio De Jeneiro nchini Brazili.

Ripoti ya pili na ya Mwisho ya madai kutoka WADA inatarajiwa kutolewa mwezi ujao juu ya udaganyifu wa Urusi katika michezo.