AFOTY: Sadio Mane alitatizwa na baridi kali Ufaransa

AFOTY: Sadio Mane alitatizwa na baridi kali Ufaransa

Sadio Mane alipowasili nchini Ufaransa mara ya kwanza, ilikuwa wakati wa majira ya baridi. Alikuwa kamwe hajaona theluji.

“Alikuwa hajakumbana na baridi kali, kwa hivyo baada ya miezi kadha, nafikiri, kwa sababu alikuwa na jeraha, hakuweza kucheza,” anasema Denis Schaeffer Mkurugenzi wa shule ya soka ya FC Metz.

Mwenyewe anakiri kwamba wakati mmoja, alifikiria kurejea nyumbani.

Lakini hakufanya hivyo, na kwa sasa ni miongoni mwa wachezaji wanaotegemewa Liverpool.

Ni mmoja wa wanaoshindania Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka 2016.