AFOTY: Yaya Toure alipovaa soksi tatu

AFOTY: Yaya Toure alipovaa soksi tatu

Yaya Toure, kiungo wa kati wa Manchester City anasema alishangaa sana alipokuwa anacheza mechi yake ya kwanza nchini ubelgiji.

"Kulikuwa na baridi kali. Saa tatu kabla ya mechi nilimwuliza meneja tungecheza vipi kwenye theluji? Nilivaa soksi tatu, kaptura tatu na shati tatu,” anasema.

Ni mmoja wa wanaoshindania Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka 2016.