AFOTY: Andre Ayew alipenda soka tangu utotoni

AFOTY: Andre Ayew alipenda soka tangu utotoni

Tangu utotoni, Andre Ayew alipenda soka. Akiwa na umri wa miaka 10 ayew alikuwa akichezea Nania FC, timu iliyomilikiwa na familia yao.

"Kwangu sina maneno ya kuelezea umuhimu wa Nania FC kwangu. Nahisi ni kila kitu. Kila wakati nikirudi nyumbani, huwa naenda huko, nafanya mazoezi nao, ni sehemu ya maisha yetu,” anasema.

Ni mmoja wa wanaoshindania Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka 2016.