AFOTY: Riyad Mahrez wakati mwingine hujificha

AFOTY: Riyad Mahrez wakati mwingine hujificha

Riyad Mahrez ameifanya timu ya taifa ya Algeria kufahamika sana na aliisaidia Leicester City kushinda taji la ligi Uingereza.

Kutokana na umaarufu wake, anasema wakati mwingine huwa vigumu kwake kutembea mitaani.

"Ni vigumu kushughulikia watu wote hawa. Najua wananipenda na mimi nawapenda, lakini siwezi kuongea na kijiji kizima," anasema.

Ni mmoja wa wanaoshindania Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka 2016.