Hector Bellerin: Arsenal atia saini mkataba mpya

Hector Bellerin Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bellerin anauguza jeraha la kifundo cha mguu

Beki wa kulia wa Arsenal kutoka Uhispania Hector Bellerin ametia saini mkataba mpya wa muda mrefu katika klabu hiyo inayocheza Ligi ya Premia.

Bellerin, 21, alijiunga na Arsenal mwaka 2011 na amekuwa mmoja wa wachezaji wa kikosi cha kwanza.

Alitia saini mkataba mwingine wa muda mrefu Julai 2015 lakini amekuwa akihusishwa na kuhamia klabu kadha, ikiwemo Barcelona alikotoka na Manchester City.

Arsenal haijatoa maelezo zaidi kuhusu mkataba wake mpya alioutia saini leo Jumatatu

"Nimekuwa hapa muda mrefu, nahisi kama hapa ni nyumbani na hili ndilo jambo bora zaidi kufanya," Bellerin amesema.

"Nina furaha, tena zaidi, kuwa Gunner kwa miaka mingi zaidi."

Bellerin amecheza mechi 67 za ligi kuu, zikiwemo 11 msimu huu.

Hata hivyo atakaa nje wiki nne baada ya kuumia akicheza dhidi ya Tottenham Hotspur.

Mada zinazohusiana