Gareth Bale kukosa mechi ya El Classico

Gareth Bale
Image caption Gareth Bale

Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale atafanyiwa upasuaji wa kifundo chake cha mguu Jumanne ijayo baada ya kuguchia katika mechi ya ushindi wa 2-1 ya vilabu bingwa Ulaya dhidi ya Sporting Lisbon.

Bale mwenye umri wa miaka 27,aliteguka katika kifundo chake cha mguu wa kulia na sasa atakosa mechi ya El Classico dhidi ya Barcelona mnamo mwezi Disemba 3.

Vyombo vya habari vya Uhispania vimeripoti kwamba raia huyo wa Wales huenda akawa nje miezi mitatu.

Mechi ya Wales inayofuata ni ya kufuzu katika kombe la dunia 2018 dhidi ya jamhuri ya Ireland mnamo tarehe 24 mwezi Machi.

Bale amechezea klabu yake na taifa mara 20 kwa jumla na kufunga mabao 11.

Aliongeza mkataba wake na Real mnamo mwezi Oktoba ambao utamweka katika klabu hiyo hadi 2022.

Viongozi wa ligi ya La Liga Real Madrid wako pointi nne mbele ya Barcelona