Bondia aliyepigwa Knockout afariki

Kuba Moczyk alifariki alipopigwa na kuanguka katika pigano lake la kwanza
Image caption Kuba Moczyk alifariki alipopigwa na kuanguka katika pigano lake la kwanza

Bondia mmoja aliyepata jeraha la kichwa katika pigano lake la kwanza amefariki.

Kuba Moczyk mwenye umri wa miaka 22 alipigwa knockout katika raundi ya tatu katika pigano la siku ya Jumamosi katika ukumbi wa Towe Complex huko Yarmouth.

Familia yake imesema kuwa alifariki siku ya Jumatano usiku katika hospitali ya James Paget huko Gorleston,ambapo amekuwa bila fahamu na kwamba amekuwa akisaidiwa na mashine.

Mkufunzi wake Scott Osinski amesema siku ya Jumatano kwamba bwana Moczyk alikuwa anaelekea kupata ushindi kabla ya kupigwa konde hilo lililomuangusha.

Mpinzani wake alikuwa na umri wa miaka 17.