Europa: Man U yashinda 4-0 Rooney ang'ara vilivyo

Juan Mata alipachika goli la pili
Image caption Juan Mata alipachika goli la pili

Mchezaji wa Manchester United Wayne Rooney amevunja rekodi kama ya magoli 39 barani Ulaya baada ya kuwashinda Feyenoord 4-0 katika mchezo wa ligi ya Europa.

Ushindi huu umeiweka Man u katika nafasi ya pili na alama 9 kwenye kundi A ikiwa nyuma ya Fernabache kwa alama moja.

Meneja wa Man U Jose Mourinho amesema kamwe milele Rooney atabaki kuwa Rooney.

Image caption Msimamo wa kundi A

Mchezo unaofuata Manchester United itamenyana na Zorya Luhansk huku ikihitaji alama moja pekee kusonga mbele

Matokeo mengine

Fenerbahçe 2-0 Zorya Luhansk

Hapoel Be'er Sheva 3-2 Inter Milan

Sparta Prague 1-0 Southampton

Dundalk 0-1 AZ Alkmaar

Zenit Saint Petersburg 2-0 Maccabi Tel-Aviv

FK Qabala 1-3 Anderlecht

FC Astana 2-1 Apoel Nicosia

FK Krasnodar 1-1 FC Red Bull Salzburg

FC Zürich 1-1 Villarreal

FC Steaua București 2-1 Osmanlispor

FC Slovan Liberec 3-0 FK Qarabag