Mourinho adaiwa kukwepa kulipa kodi

Mkufunzi wa manchester United Jose Mourinho
Maelezo ya picha,

Mkufunzi wa manchester United Jose Mourinho

Mbunge mmoja nchini Uingereza amesema kuwa mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anafaa kuchunguzwa na maafisa wa Uingereza kufuatia madai kwamba alitumia kampuni za kigeni kupunguza kodi anayolipa.

Mourinho anashtumiwa kwa kuhamisha mamilioni ya pauni za Uingereza hadi kisiwa kinachomilikiwa na Uingereza cha Virgin Island ili kukwepa kulipa kodi.

Hatahivyo ajenti wa mkufunzi huo amesema kuwa madai hayo hayana msingi wowote.

Mwenyekiti wa kamati ya hesabu za mali ya umma Meg Hillier aliambia Gazeti la Sunday Times kwamba madai hayo yanafaa kuchunguzwa.

Shirika la mapato na kodi nchini humo limesema kuwa halitatoa tamko lolote kuhusu watu waliotajwa ,lakini linachukulia madai yote ya kukwepa kulipa kodi na umuhimu mkubwa na kwamba litachunguza madai ya udanganyifu pamoja ushahidi unaotolewa.