Man U waingia hatua ya mtoano

Henrikh Mkhitaryan aibeba Manchester
Image caption Henrikh Mkhitaryan aibeba Manchester

Manchester United wameingia katika hatua ya mtoano ya Europa League kwa kuichapa Zorya Luhansk ya Ukrain.

Ilikuwa Henrikh Mkhitaryan ambaye amefungua dimba dakika ya 48 kwa kuipatia Manchester goli la kwanza. Henrikh alinunuliwa kwa pauni million 26 na kabla ya kuhamia Manchester alikuwa ametangazwa kuwa Mchezaji wa msimu wa Bundesliga ingawa Mourinho amekuwa hamtumii mara kwa mara sana. La pili limefungwa na Ibrahmovic dakika ya 88.

Southampton wametolewa katika Europa League baada ya kutoka Sare na Hapoel Beer Sheva. Southampton walikuwa wanahitaji kupata sare ya bila magoli lakini dakika 15 kabla ya mchezo kufika mwisho Maor Buzaglo anautibua mpango wao na wao wanalazimika kusawazisha katika dakika ya 90 kupitia kwa Virgil van Dijk, lakini ni katika muda ambao wanakosa nafasi ya kuongeza la pili.