Europa League: Man Utd kukutana na St-Etienne, Giurgiu v Genk

Jose Mourinho Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mourinho alishinda kombe hilo lilipokuwa linaitwa Kombe la Uefa Cup akiwa na Porto msimu wa 2002-03

Manchester United watakutana na klabu ya Saint-Etienne ya Ufaransa katika hatua ya 32 bora ligi ndogo ya Ulaya, Europa League nao Tottenham Hotspur wakutane na Gent ya Ubelgiji.

Klabu ya Genk ya Ubelgiji, anayoichezea Mtanzania Ally Samatta, itakutana na Astra Giurgiu ya Romania.

Kiungo wa Manchester United Paul Pogba atakutanishwa na ndugu yake mkubwa Florentin, anayechezea Saint-Etienne ambao kwa sasa wamo nambari nane Ligue 1.

Spurs hawajawahi kukutana na Gent, ambao walimaliza wa tatu ligi kuu ya Ubelgiji msimu uliopita.

Kwenye droo hiyo, klabu za Ligi ya Premia hazingepangwa pamoja, sawa na klabu kutoka taifa moja.

Fainali ya Europa League itachezewa uwanja wa Friends Arena mjini Stockholm mnamo 24 Mei.

Pogba vPogba

Haki miliki ya picha Instagram
Image caption Beki wa Saint-Etienne Florentin Pogba alipakia mtandaoni picha hii mseto yake na kakake Paul na kuandika : Pogba (v) Pogba

Kuhusu Paul Pogba kucheza dhidi ya kakake Florentin, 26, Mourinho alisema: "Ni jambo zuri. Paul atakuwa akicheka sana, na najua nduguye atakuwa anacheka pia. Ni jambo zuri, ambalo limefanyika mara chache sana katika historia ya soka."

Droo kamili

Athletic Bilbao (Uhispania) v Apoel Nicosia (Cyprus)

Legia Warsaw (Poland) v Ajax (Uholanzi)

Anderlecht (Ubelgiji) v Zenit St Petersburg (Urusi)

Astra Giurgiu (Romania) v Genk (Ubelgiji)

Manchester United (England) v Saint-Etienne (Ufaransa)

Villarreal (Uhispania) v Roma (Italia)

Ludogorets (Bulgaria) v FC Copenhagen (Denmark)

Celta Vigo (Uhispania) v Shakhtar Donetsk (Ukraine)

Olympiakos (Ugiriki) v Osmanlispor (Uturuki)

Gent (Ubelgiji) v Tottenham Hotspur (England)

Rostov (Urusi) v Sparta Prague (Czech Republic)

Krasnodar (Urusi) v Fenerbahce (Uturuki)

Borussia Monchengladbach (Ujerumani) v Fiorentina (Italia)

AZ Alkmaar (Uholansi) v Lyon (Ufaransa)

Hapoel Beer Sheva (Israel) v Besiktas (Uturuki)

PAOK (Ugiriki) v Schalke (Ujerumani)

Mada zinazohusiana