Chelsea na Manchester City wapigwa faini

Cesc Fabregas na Fernandinho

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Fernandinho alifukuzwa kwa kumkaba koo Cesc Fabregas

Chelsea wamepigwa faini ya £100,000 na Manchester City wakapigwa faini ya £35,000 baada ya wachezaji wao kuhusika katika vurugu uwanjani wakati wa mechi ya Ligi ya Premia.

Hisia zilipanda na wachezaji wakakabiliana mechi hiyo iliyochezewa uwanjani Etihad ilipokaribia kumalizika baada ya Sergio Aguero wa City kufukuzwa uwanjani kwa kumchezea visivyo beki wa Chelsea David Luiz.

Fernandinho pia alifukuzwa uwanjani kwa kumkaba koo Cesc Fabregas wachezaji wa klabu hizo mbili walipokabiliana baada ya kisa hicho.

Chelsea walishinda 3-1.

Blues walikuwa awali wametahadharishwa kwamba wanaweza kupokonywa alama kwa utovu wa nidhamu.

Viongozi hao wa Ligi ya Premia wamepigwa faini mara sita tangu Februari 2015 kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji.

Maelezo ya picha,

Klabu ambazo Chelsea walikuwa wanacheza dhidi walipopigwa faini tangu Februari 2015

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Arsenal walipokonywa alama mbili nao Manchester United moja baada ya vurugu uwanjani 1990