Man City kupepetana na Arsenal EPL

Man City kukabiliana na Arsenal EPL Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Man City kukabiliana na Arsenal EPL

Kiungo wa kati wa Manchester City IIkay Gundogan huenda akawa nje kwa miezi kadhaa baada ya kupata jeraha la goti wakati wa mechi dhidi ya Watford.

City itaendelea kuwakosa Fernandinho na Sergio Aguero ambao wanahudumia marufuku.

Mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck anatarajiwa kurudi katika mazoezi wiki ijayo baada ya kuuguza jeraha la goti kwa miezi kadhaa.

Aaron Ramsey na Shkodran Mustafi bado wanauguza majeraha pamoja na Peter Mertesacker na Santi Carzola.