Crystal Palace yamfuta kazi meneja Allan Pardew

Mkufunzi wa Crystal palace Allad Pardew amepigwa kalamu
Image caption Mkufunzi wa Crystal palace Allad Pardew amepigwa kalamu

Klabu ya Crystal Palace imemfuta kazi mkufunzi wake Alan Pardew wakati ambapo klabu hiyo iko katika nafasi ya 17 katika ligi ya Uingereza.

Pardew aliteuliwa na kupewa kandarasi ya miaka mitatu na nusu katika mkataba uliotiwa sahihi mnamo mwezi Januari 2015, lakini meneja huyo mwenye umri wa miaka 55 amefutwa kazi baada ya kushinda mechi moja pekee kati ya 11.

Palace imejipatia pointi 26 kutoka mechi 36 ilizocheza 2016 na iko pointi moja tu juu ya timu zilizo katika hatari ya kushushwa daraja.

Aliyekuwa kocha wa Uingereza Sam Allardyce anapigiwa upatu kuchukua wadhfa huo.