Mourinho: Schneiderlin anaweza kuondoka

Morgan Schneiderlin kulia
Image caption Morgan Schneiderlin kulia

Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa yuko tayari kumruhusu kiungo wa kati wa Ufaransa Morgan Schneiderlin kuondoka katika klabu hiyo baada ya mchezaji huyo kutaka kufanya hivyo.

''Siwezi kumzuia mchezaji ambaye hana raha.Ingekuwa rahisi kumkataza iwapo ningekuwa namshirikisha kila mechi lakini kwa sababu anashiriki mara moja moja, basi sina budi kumwachilia kwenda iwapo ombi linaloletwa kwa Manchester United linavutia''.

Schneiderlin mwenye umri wa miaka 27 aliisaidia klabu ya Southampton katika mikutano kadhaa kati ya klabu hizo mbili hatua iliolazimu Manchester United kumsajili.