Liverpool yatoana jasho na Manchester City uwanjani Anfield

MKufunzi wa Manchester City Pep Guardiola akizungumza na Jurgen Klopp wa Liverppol wakati wawili hao walipokuwa wakifunza Bayern Munich na Burusia Dortmund nchini Ujerumani
Image caption MKufunzi wa Manchester City Pep Guardiola akizungumza na Jurgen Klopp wa Liverppol wakati wawili hao walipokuwa wakifunza Bayern Munich na Burusia Dortmund nchini Ujerumani

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anasema kuwa Phillipe Coutinho anaendelea kupata nafuu katika jeraha la kifundo cha mguu lakini anatarajia kwamba hatoshiriki katika mechi mbili zijazo.

Beki Joel Matip pia anaguzua jeraha kama hilo.

Mshambuliaji wa wa Manchester City Sergio Aguero atashiriki katia mechi dhidi ya manchester City baada ya kuhudumia marufuku ya mechi nne.

Beki John Stones pia huenda akashiriki baada ya kupona jeraha la goti ,lakini Leroy Sane na Vincent Kompany bado wanaendelea kuuguza majeraha.

Mkufunzi wa Liverpool amesema: Manchester City wana wachezaji wazuri uwanjani na wachezaji wazuri katika benchi.

Naye Pep Guardiola amesema kuwa Liverpool ni miongoni mwa timu ambazo zitapigania taji la ligi msimu huu.