Liverpool yaizidi ujanja Manchester City

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp na mwenzake wa Manchester City Pep Guardiola Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp na mwenzake wa Manchester City Pep Guardiola

Klabu ya Liverpool iliendeleza juhudi zake za kutaka kushinda taji la ligi ya Uingereza na kupanda hadi pointi sita nyuma ya viongozi wa ligi Chelsea kupitia ushindi wao dhidi ya Manchester City.

Georginio Wijnaldum alifunga bao kunako dakika ya nane kutoka kwa krosi iliopigwa na Adam Lallana ili kuiweka Liverpool katika nafasi ya pili ya jedwali la ligi katika uwanja wa Anfield.

Mkufunzi wa Liverpool aliongoza sherehe za ushindi huo mwisho wa mechi iliokuwa na visa vingi.

City waliotafuta bao kwa udi na uvumba waliimarika katika kipindi cha pili lakini hawakumtishia kipa wa Liverpool Simon Mignolet na kushindwa kwao kunawawacha pointi 10 nyuma ya Chelsea.

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema bado hajafikiria kwamba huenda akashinda ligi na anasema kwamba atakuwa na hamu ligi inapokamilika

Mada zinazohusiana