Mkuu wa mchezo wa Kriketi India apigwa kalamu

Anurag Thakur Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Anurag Thakur

Mahakama kuu nchini India imemsimamisha kazi mkuu wa halmashauri kuu ya kusimamia mchezo wa Kriketi nchini humo Anurag Thakur, kwa kushindwa kuiletea bodi hiyo mageuzi yafaayo.

Bodi hiyo ya kriketi ni maarufu sana nchini India.

Bwana Thakur amejibu hatua hiyo ya mahakama huku akisema kuwa halmashauri ya kusimamia mchezo wa kriketi ni moja ya shirikisho bora zaidi nchini humo.

Miaka miwili iliyopita, katika kashfa kubwa ya ufisadi, mahakama hiyo iliteuwa kamati maalum, ya kupigia msasa maswala ndani ya BCCI inavyoendeshwa.

Mwezi Julai mwaka jana, mahakama iliiamuru halmashauri hiyo kuu kuleta mabadiliko, jambo ambalo linalaumiwa kuwa halikutekelezwa.