Leicester City kumchukua mchezaji wa Nigeria Wilfred Ndidi

Wilfred Ndidi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndidi aliwasaidia Genk kufika hata ya muondoano Europa League

Leicester City wanatarajiwa kumnunua kiungo wa kati wa klabu ya Genk ya Ublegiji Wilfred Ndidi kwa £15m.

Klabu hizo tayari zimeafikiana kuhusu kuhama kwake na kilichosalia pekee ni kibali chake cha kufanyia kazi Uingereza.

Chipukizi hiyo wa miaka 20 kutoka Nigeria atatia saini mkataba wa miaka mitano unusu atakapokamilisha uhamisho wake.

Leicester, kwenye tovuti yao, wamethibitisha kwamba klabu hizo zimeafikiana na kwamba Ndidi amefanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

"Ndidi anatarajiwa kukamilisha utaratibu wa kuhamia kamili Leicester City baadaye wiki hii."

Ndidi aliwasaidia Genk kumaliza wa kwanza kundi lao la Europa League msimu huu na kufuzu kwa hatua ya muondoano.

Mada zinazohusiana