Rooney asawazisha mabao na Bobby Charlton

Maelezo ya video,

Rooney asawazisha mabao na Bobby Charlton

Wayne Rooney amasawazisha idadi ya mabaoa na ya Sir Bobby Charlton ambaye aliwezk rekodi ya kufunga idadi kubwa zaidi ya mabao akichezea klabu ya Manchester United.

Rooney mwenye umri wa miaka 31 alifunga bao wakati wa mchuano kati ya Manchester United na Reading na kufikisha jumla ya mabao 249 kwa mechi 543.

Rekodi hiyo ya Charlton imekuwepo tangu mwaka 1973.

Mwaka 2015 Rooney alivunja rekodi ya Charlton ya mabao 49 aliyofungia timu ya England na kuongeza idadi hiyo hadi mabao 53.

Rooney alionyesha dalili za kuvunja rekodi hiyo tangu mwanzo, alipohamisha taaluma yake hadi Old Trafford.

Wakati wa mechi yake ya kwanza alipoihama Everton kwa kima cha pauni milioni 27 mwaka 2004 alifunga bao dhidi ya Fenerbahce

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Rooney aliihama Everton kwa kima cha pauni milioni 27 mwaka 2004

Maelezo ya picha,

Jinsi Rooney alifunga mabao yake