Fifa: Bao bora duniani lilitoka Malaysia

Mohd Faiz Subri Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mohd Faiz Subri ndiye raia wa kwanza wa Malaysia kushinda tuzo hiyo

Mchezaji kandanda kutoka Malaysia Mohd Faiz Subri ameshinda Tuzo ya Puskas inayotolewa na FIFA kwa mfungaji wa bao bora zaidi wa mwaka.

Faiz, anayechezea klabu ya Penang FA ndiye raia wa kwanza kabisa wa Malaysia kuwa mshindi wa tuzo hiyo.

Mchezaji huyo wa miaka 29 kutoka Penang alipata karibu asilimia 60 ya kura zilizopigwa kwa bao lake la frikiki alilofunga mechi ya Ligi Kuu ya Maaysia dhidi ya timu ya Pahang mwezi Februari

Alikabidhiwa tuzo hiyo na mchezaji soka mahiri kutoka Brazil, Ronaldo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Faiz akikabidhiwa tuzo yake na Ronaldo

Waliokuwa wanashindania tuzo hiyo mwaka huu ni Marlone na kiungo wa kati wa Venezuela Daniuska Rodriguez.

Cristiano Ronaldo wa Ureno na Real Madrid alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka duniani na kumshinda Lionel Messi wa Barcelona na Argentina.

Mada zinazohusiana