Mwana wa Patrick Kluivert, Justin, aichezea Ajax ya Uholanzi

Justin Kluivert (upande wa kushoto) Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Justin Kluivert (upande wa kushoto)

Mtoto wa mshambuliaji wa Uholanzi Patrick Kluivert, Justin, mwenye umri wa miaka 17 amejitosa kwa mara ya kwanza uwanjani akiwa na klabu ya Ajax na kupata ushindi katika ugenini PEC Zwolle siku ya Jumapili.

Winga Kluivert aliingia uwanjani katika dakika ya 39 baada ya Amin Younes kuumia.

Mkwaju wa penalti kutoka kwa Lasse Schone uliiweka Ajax mbele na Hakim Ziyech akaongeza la pili.

Nicolai Brock-Madsen alikomboa goli moja lakini Ziyech akaongeza jingine na kuwahakikishia Ajax ushindi ambao unaifanya Ajax kusalia na alama tano nyuma ya viongozi Feyenoord, iyoichapa Roda 2-0.

Babake, Kluivert Sr, alishinda mataji mawili ya Eredivisie ya uholanzi na pia akashinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya alipokuwa akichezea klabu ya Ajax kwa miaka mitatu kati ya mwaka 1994 na 1997

Alienda kuichezea AC Milan, Barcelona, Newcastle United, Valencia, PSV Eindhoven na Lille na alifunga magoli 40 katika mechi 79 alizochezea taifa lake.

Kiungo huyo ambaye kwa hivi sasa ana umri wa miaka 40 ni mkurungezi wa mpira wa soka katika klabu ya PSG. ya Ufaransa

Mada zinazohusiana