Ghana yailaza Uganda

Nahodha wa kikosi cha Ghana Asamoah Gyan kulia aliyepata penalti Haki miliki ya picha Justin Tallis
Image caption Nahodha wa kikosi cha Ghana Asamoah Gyan kulia aliyepata penalti

Andre Ayew alifunga bao la pekee la mechi dhidi ya Uganda katika mechi ya ufunguzi ya kundi D katika michuano ya kombe la bara Afrika linaloendelea nchini Gabon.

Winga huyo wa klabu ya West Ham alifunga bao la penalti kunako dakika ya 32 baada ya nahodha Asamoah Gyan kuvutwa katika eneo la hatari.

Ghana pia ilitishia kupitia vichwa viwili vya Gyan ,huku Ayew na Christian Atsu wakimjaribu kipa wa Uganda Denis Onyango.

Uganda walikaribia lango la Ghana baada ya Faruku Miya kupiga mwamba wa goli lakini hawakuweza kusawazisha.

Uganda wanaocheza kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978 hawakuwa na bahati.

Cranes walitengeza fursa chache na walishindwa kuingia katika lango la Ghana ambao walifurahia kulinda lango lao .