Jesus aisaidia Manchester City kuishinda Swansea

Gabriel Jesus Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gabriel Jesus

Gabriel Jesus alifunga mara mbili likiwemo bao la dakika za ziada na kuiwezesha Manchester City kusonga hadi nafasi ya tatu kwenye ligi kuu katika mechi kali dhid ya Swansea uwanjani Etihad.

Manchester City iliitawala Mechi kipindi cha kwaza likini wao nao walionekana kupata nguvu kipindi cha pili.

Manchester City ilifunga bao lake la kwanza dakika ya 11 baada ya Gabriel Jeses kupata mpira kutoka kwa Raheem Sterling.

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Sasa Juses ameifungia Man City mabao 3 kweney mechi mbili tangu ajiunge nao akitokea Palmeiras.

Sasa Juses ameifungia Man City mabao 3 kweney mechi mbili tangu ajiunge nao akitokea Palmeiras.

Changamoto sasa kwa kikosi hiki cha Pep Guardiola ni kuteatea mwendo huu.