Argentina yazidi kung'ara viwango bora vya soka Duniani-Fifa

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Shirikisho la soko duniani

Shirikisho la soka Ulimwenguni (FIFA) hapo jana limetoa orodha mpya ya ubora wa viwango vya soka Duniani kwa nchi Wanachama , na Vinara wake bado ni Argentina wakifuatia Brazil na kwa Afrika ni Misri ndio wapo juu kabisa huku Tanzania ikishuka Nafasi 2 na kukamata Namba 158.

5 Bora kwenye orodha hiyo zimebaki zile zile bila mabadiliko na nazo ni Argentina (1), Brazil (2), Germany (3), Chile (4) na Belgium (5).

Kwa Afrika, Nchi ambayo iko juu kabisa ni Misri, waliotolewa Fainali ya AFCON 2017, ambao sasa wapo Nafasi ya 23 baada kupanda Nafasi 12 wakifuata Senegal walio Nafasi ya 31 na Mabingwa Wapya wa Afrika ambao ni Cameroon, wapo Nafasi ya 33 baada kupaa Nafasi 29.

Orodha hiyo ni;

 1. Argentina
 2. Brazil
 3. Germany
 4. Chile
 5. Belgium
 6. France
 7. Colombia
 8. Portugal
 9. Uruguay
 10. Spain
 11. Switzerland
 12. Wales
 13. England
 14. Poland
 15. Italy
 16. Croatia
 17. Mexico
 18. Peru
 19. Costa Rica
 20. Iceland

Kwa upande wa Afrika Uganda bado wanaendelea kuongoza kwa Afrika Mashiriki wakiwa nafasi ya 17 kwa Afrika na 75 duniani wakifuatiwa na Kenya waliopo nafasi ya 20 Afrika na 87 duniani wakati Rwanda wako nafasi ya 27 Afrika na 100 duniani na Burundi nafasi ya 40 Afrika na 138 duniani

Kwa upande wa Afrika Misri wamekuwa vinara kwa kukwea kwa nafasi 12 na kutua kileleni wakiwa nafasi ya 23, wakifuatiwa na Senegal walioko nafasi ya 31 huku mabingwa wa michuano ya Mataifa ya Afrika Cameroon nao wakikwea kwa nafasi 29 mpaka nafasi ya 33 duniani.