Conte hapendi "mzaha" wa Mourinho

Mourinho na Conte Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mourinho na Conte

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anasema hapendi mzaha wa meneja wa Manchester United Jose Mourinho, baada ya Mourinho kusema kuwa Chelsea hucheza mchezo wa kujilinda tu.

Chelsea iko kileleni na pointi 10 baada ya mechi ya Jumapili ambapo walitoka sare ya bao moja na Burnley.

Mourinho ambaye anafahamika kwa kuwafanyia mzaha mahasimu wake, alisema kuwa klabu hiyo yake ya zamani haiwezi kuimarisha mchezo wao kwa sababu wao hushinda kwa kujibu mashambulizi.

Mourinho alikuwa akiongea baada ya Manchester United kuwashinda Watford mabao 2-0 siku ya Jumamosi na kuweka rekodi yao ta kutoshindwa hadi mechi 16. Man U wako nafasi ya sita katika jedwali la ligi pointi 12 nyuma ya Chelsea.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Chelsea beat waliwashinda Manchester United 4-0 mweiz Oktoba