Man City ina matumaini ya Jesus kurudi uwanjani

Gabriel Jesus Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Gabriel Jesus alikuwa mbioni kufunga bao kila mechi katika mechi zake za tatu za kwanza Manchester City

Manchester City wanamatumaini kuwa kiungo wa mbele Gabriel Jesus, hakupata jeraha baya la mguu wakati wa mechi yao waliyowashinda Bournemouth mabao 2-0.

Jesus mwenye umri wa miaka 19 alifunga mabao katika mechi mbi za kwanza tangu ajiunge Ciry, lakini alicheza tu dakika 14 wakati wa mechi na Bournemout kufuatia jeraha.

Man City watabainisha hali ya jereha lake leo Jumanne.

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Gabriel Jesus

Tunamatumaini kuwa halitakuwa tatizo kubwa, meneja wa City Pep Guardiola aliiambia BBC.

Jesus ambaye alitokea Palmeiras mwezi Januari, alifunga mabao ya ushindi wakati walipokutana na West Ham na baadaye Swansea na alikuwa mbioni kuwa mchezaji wa tatu wa city baada ya Emmanuel Adebayor na Kevin de Bruyne, waliofunga mabao wakati wa mechi zao tatu za kwanza mara baada ya kujunga na Man City.

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Gabriel Jesus alikuwa mbioni kufunga bao kila mechi katika mechi zake za tatu za kwanza Manchester City