Ancelotti: Arsene Wenger anafaa kupongezwa

Arsene Wenger
Image caption Arsene Wenger

Mkufunzi wa klabu ya Bayern Munich Carlo Ancelotti amesema kuwa anamuheshimu mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger na akasema kuwa mkufunzi huyo ataweza kujinasua kutoka kwa shutma ambazo zimekuwa zikimkabili hivi majuzi.

Matokeo mabaya katika ligi ya Uingereza yameongeza uvumi kuhusu hatma ya raia huyo wa Ufaransa huku baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wakimtaka aondoke.

Ancelotti anaamini kwamba Wenger anafaa kupongezwa kwa kazi aliyofanya.

''Alijenga kitambulisho na mbinu nzuri ya kusakata soka'' ,alisema raia huyo wa Itali.

''Wenge ana uzoefu wa kujua kwamba katika kazi yetu ni swala la kawaida kukosolewa.

Image caption Carlo Ancelotti

kwa hilo hana tatizo. Ninaheshimu sana kazi aliyofanya katika klabu ya Arsena''l.

Ancelotti ambaye aliwahi kuifunza Chelsea alikuwa akizungumza kabla ya mechi ya Jumatano ya klabu bingwa ya awamu ya kwanza kati ya timu hizo mbili nchini Ujerumani.