Carli Lloyd ajiunga na Man City

Ulaya Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Carli Lloyd

Timu ya Manchester City ya wanawake imemsajili mchezaji bora wa dunia kwa upande wa wanawake Mmarekani Carli Lloyd kwa mkataba wa muda mfupi.

Nyota huyu ataitumika Man City katika michuano ya klabu bingwa na kombe la Fa na mkataba wake utafika ukomo June 3 mwaka huu.

Lloyd mwenye umri wa miaka 34 anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji amefunga jumla ya magoli 96 katika michezo 232 ya kimtaifa.

Nahodha huyu wa timu ya taifa ya Marekani ni mchezaji wa tatu kujinga na ligi ya England baada ya Wamarekani wenzake winga Crystal Dunn kujiunga na Chelsea na kiungo Heather O'Reilly kujiunga na Arsenal