Ndugu wa Pogba kukutana ugani Old Trafford leo

Florentin Pogba na Paul Pogba Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Florentin Pogba na Paul Pogba

Mchezaji wa kimataifa wa Guinea Florentin Pogba, anasema kuwa itakuwa changamoto kuwa mama yake kutazama mechi wakati anakutana na klabu anayoichezea nduguye mdogo Paul Pogba katika ligi ya Europa

Leo Alhamisi St Etienne anayoichezea Florentina Pogba, watakutana na Manchestetr United huko Old Trafford.

"Hautakuwa wakati rahisi lakini pia utakuwa wakati wa kipekekee kwa mama kutazama vijana wake wakicheza," Florentin alisema.

"Labda angependa tutoke sare."

Paul mwenye umri wa miaka 23 ndiye mchezaji ghali zaidi duniani baada ya kujiunga na Manchester United kwa kima cha pauni milioni 111 kutoka kwa mabingwa wa Italia Juventus na anaiwakilisha Ufaransa alikozaliwa.

Florentina ambaye alizaliwa mjini Conakry kabla ya wazazi wake kuhamia Ufaransa ameichezea St Etiene tangu mwaka 2012, na kwanza aliichezea Guinea mwaka 2010.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Kabla ya mechi Florentin amachora kichwani namba 19 ambayo ni namba yake ya jesi,m na namba 6 ambayo ya nduguye Paul Pogba