Florentin Pogba kukabiliana na nduguye Paul Pogba

Ndugu wawili Florentin Pogba na Paul Pogba Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ndugu wawili Florentin Pogba na Paul Pogba

Mchezaji wa kimataifa wa Guinea Florentin Pogba amekiri kuwa mamake atakuwa katika hali ngumu wakati atakapotazama akimkabili nduguye mdogo Paul katika mechi ya ligi ya Europa.

Siku ya Alhamisi Florentin ataichezea St Etienne dhidi ya Paul Pogba anayechezea Manchester United.

''Haitakuwa rahisi kwake lakini ni wakati muhimu kuwaona wanawe wakicheza'' ,alisema beki huyo.

''Pengine matokeo mazuri kwake itakuwa sare, lakini sote wawili tutajitolea kuona kwamba tunapata matokeo mazuri kwa timu zetu. Yeyote atakayeibuka mshindi atafurahia''.

Mechi ya siku ya Alhamisi itakuwa ya kwanza kwa ndugu hao wawili waliokulia karibu na mji mkuu wa Ufaransa Paris, watapambana katika uwanja wa soka.