Chelsea waitandika Wolves mabao 2-0

Pedro alifunga bao lake la nne la FA msimu huu

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha,

Pedro alifunga bao lake la nne la FA msimu huu

Viongozi wa ligi kuu wa Primia Chelsea wamefika robo fainali ya kombe la FA baada ya kuwashinda Wolves mabao 2-0 katika mechi ya kusisimua iliyoandaliwa kwenye uwanja wa Molineux.

Wolves walionyesha mchezo mzuri na kuishambulia ngome ya Chelsea mara kwa mara kabla ya wageni kuamka na kuwasukuma wenyeji nyuma.

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha,

Fabregas alikuwa mchangamfu na alichangia pakubwa mashambulizi ya Chelsea

Diego Costa aliifungua Chesea bao la pili na kufikisha jumla ya mabao 16 msimu huu.

Chelsea ambao wamefungu mwanya wa pointi 8 wakiwa kileleni mwa jedwali, walikumbana na shinikizo kali kutoka kwa Burnely walipotoka sare ya bao 1-1 wiki iliyipiya.