Nyota wa Afcon ajiunga na klabu ya China

Christian Bassogog,Mchezaji bora wa kombe la Afrika,2017

Chanzo cha picha, Google

Maelezo ya picha,

Christian Bassogog,Mchezaji bora wa kombe la Afrika,2017

Kiungo wa kati wa Cameroon Christian Bassogog, amejiunga na klabu ya China ya Henan Jianye, inayoshiriki michuano ya ligi kuu ya Uchina kutoka klabu ya Aab Fodbold.

Mapema mwezi huu shambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alitajwa kuwa mchezaji bora wa Afcom baada ya Cameroon kupata ushindi wao wa tano kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya kombe la Taifa nchini Gabon.

Aab imemuuza Bassogog kwa klabu ya Henan Jianye FC kwa rekodi ya uhamisho kuelekea Aab, klabu hiyo imesema katika taarifa yake.

Bassogog amesema pendekezo la China hangeweza kulikataa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Christian Bassogog

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon alishiriki mechi zote sita katika Kombe la Mataifa , na kufunga bao katika hatua ya nusu fainali pale Indomitable Lions walipowachapa Ghana 2-0.

Kwa sasa anakuwa miongoni mwa wachezaji wa kiafrika kuelekea Uchina , baada ya mchezaji wa Nigeria John Mikel Obi na Odion Ighalo walipojiunga na Tiajin Teda na Changchun Yatai mtawalia mwezi uliopita.