Balotelli atimuliwa uwanjani kwa mara ya tatu msimu huu

Mario Baloteli
Maelezo ya picha,

Mario Baloteli

Mshambuliaji wa Nice Mario Balotelli alitolewa uwanjani kwa mara ya tatu msimu huu, lakini timu yake ya Nice ilipata ushindi 1-0 dhidi ya klabu ya Lorient katika Ligue 1.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool alitolewa uwanjani katika dakika ya 68 baada ya kumchezea vibaya ikabu Zargo Toure.

Bao la Wylan Cyprien, liliwapatia wageni hao uongozi katika dakika ya 15 na kuwapatia ushindi wa kwanza katika mechi walizoshiriki ugenini tangu mwezi Novemba.

Nice wamesongea katika nafasi ya pili na alama tatu, nyuma ya Monaco, waliotoka sare ya 1-1 dhidi ya Bastia siku ya Ijumaa.

Upande wa Lucien Favre wako mbele ya Paris St-Germain ,ambao watarudi katika nafasi ya pili iwapo hawatakubali kufungwa nyumbani watakapokabiliana na Toulouse siku ya Jumapili.

Balotelli , ameifungia klabu yake ya Nice magoli 11 tangu kuwasili kwake kutoka Liverpool msimu uliopita.

Balotelli alitolewa baada ya kupokea kadi mbili za manjano mara mbili katika mechi iliyopita dhidi ya Lorient mwezi Oktoba.

Pia alipokea kadi nyekundu walipotoka sare na Bordeaux mwezi Disemba.

Clinton N'Jie na Florian Thauvin waliifungia Marseille.