Manchester City v Monaco: Pep Guardiola wakosoaji 'wataiua 'City tukishindwa

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola anataka wachezaji wake wahimili matarajio ya hatua ya timu 16 bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya watakapokabiliana na Monaco jioni licha ya kuwa "wakosoaji watawaua", iwapo watalazwa

Meneja huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich, Pep Guardiola, ameshinda taji hilo mara mbili kama kocha na hakufeli kuifikisha timu hizo katika nusu fainali mara saba.

"Kufika hapa si rahisi," alisema Guardiola

"Nataka kuwahimiza wachezaji wafurahie wakati huu. Ni wakati mzuri.''

City walifika katika hatua ya nusu fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara ya kwanza msimu uliopita na wameendelea katika hatua ya muondoano mara nne pekee.

Watu wanaweza kufikiria Manchester City wanastahili kuwa hapa lakini klabu nyingi kubwa hazijafika hapa, amesema Guardiola mwenye umri wa miaka 46 .

''Sisi tuna bahati,''Guardiola

"Historia ya hivi majuzi ni nzuri lakini katika historia ya muda mrefu, Manchester City haijakuwa katika nafasi hii kwa muda."

"Bara lote litatatutazama, kutuchambua, ili kutuua, iwapo hatutashinda ama watasema jinsi tulivyoonyesha mchezo mzuri iwapo tutashinda."

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kevin de Bryune

Kiungo wa kati wa City Kevin de Bruyne anarudi uwanjani akiwa amefunga magoli matano katika mechi 32 alizoshiriki msimu huu.

Bryune alitoka Wolfburg kwa kitita cha pauni milioni 55 mwezi Agosti mwaka 2015 ambapo alikuwa amefunga magoli 18 katika michezo aliyoshiriki na klabu hiyo.